Bara la Amani

Bara la Amani

Bara la Amani

Maiko na Rashidi walipanda treni wakirudi London, na baada ya treni kuondoka Maiko alianza kumwambia Rashidi:

Katika mazungumzo yako umekuwa unakumbusha mara kwa mara pointi muhimu sana ambayo naona hukuipa haki yake, mara nyingi ulikuwa ukisema: “Lengo la kuumbwa mwanadamu” na nakumbuka kuwa ulitaja mara moja kuwa lengo hilo ni kumuabudu Mungu, suala hili linanishughulisha sana na linawashughulisha na wale ninaowafahamu, mara nyingi mtu anakutana na matukio anajiuliza. Kwa nini mimi nipo katika dunia hii? Kwa nini tabu na mashaka yote? Kwa nini mgongano huu baina ya wanadamu, bali baina ya mwanadamu na ulimwengu? Je haya sio maswali muhimu?

Rashidi: Ndio, bila shaka ni muhimu, nami nadhani hilo linarejea katika mfumo wa maadili ya mtu wa Magharibi na utamaduni wake, hatima ya mgongano huo ni moja ya misingi muhimu ambayo juu yake unasimama utamaduni wa maada wa Ki-Magharibi, nayo imetoka katika staarabu mbili za zamani za Kiyunani na Kiroma ambao leo hii ustaarabu wa Kimagharibi umesimama katika nguzo zake ambayo hatima ya mgongano ni moja katika fikra za msingi katika staarabu mbili hizi: mgongano kati ya miungu, na mgongano kati ya wanadamu na Mungu na mgongano kati ya mwanadamu na mazingira, na mgongano kati ya nguvu ya shari na nguvu ya kheri, nyongeza ya faragha ya kiroho inayotokana na muelekeo wa kimaada ambao ustaarabu wa Ki-Magharibi leo hii umejitambulisha nao.

Maiko: Wewe unazungumza kama kwamba unamiliki sifa ya ufasaha ya kumvutia mtu unachotaka kumpa.

Rashidi: Jambo hili kwa Muislamu mwenye imani sahihi haliwezi kumkanganya; Muislamu anafahamu kwa Uislamu wake: Ametokea wapi, anakwenda wapi, nini thamani yake na ni kazi gani aliyo nayo mwanadamu?

Maiko: Bado swali langu lipo, bali umeniongezea maswali mengine mengi, ni ipi taswira ya Uislamu kujibu maswali haya?

Rashidi: Muislamu siku zote yupo katika muafaka na ulimwengu huu na vipengele vyake na kuwa vitu hivi vinashirikiana na mja mwema katika kumnyenyekea Mwenyezi Mungu na kumtukuza, kwa hakika katika sura ya uchaguzi na jinsi ilivyo ipo wazi kama ilivyo katika ulimwengu wetu wa wanadamu, au kwa sura halisi ya kimaumbile ama namna gani hilo halijulikani kwetu….Mara nyingi Qur’an imerejea utajo kuwa “Aliyemo duniani anamtukuza Mwenyezi Mungu.” Maneno haya yamekuja zaidi ya mara thelathini kwa tamshi “Kutukuza” na maana hii imerejea kinyume cha tamshi “Kusabihi” mara nyingi vile vile. Hivyo basi Muislamu mwenye utambuzi hufahamu ya kuwa yeye ni (kiungo) mwanachama katika timu ya nyimbo ya ulimwengu huu ambayo inamtukuza Mwenyezi Mungu Mtukuka, yeye yupo katika hali ya kuafikiana na ulimwengu huu na vipengele vyake na sio katika hali ya kupambana na kuchukizana.

Kama ambavyo huhisi mazoea ya kitabia na liwazo, na huona urafiki na sio uadui; kwani Qur’an imesema kuwa yaliyomo ulimwenguni yote yamedhalilishwa kwa mwanadamu, na kwa tamshi hili limekuja zaidi ya mara ishirini na kwa matamko mengine zaidi ya hivyo.

Maiko: Kuna nini nyuma yake! Nini kinachopelekea hilo?

Rashidi: Tukiangalia: anachokihitaji mwanadamu ili moyo wake utulie na hivyo kumpelekea katika furaha na kuishi katika utu wake……yote tunaona yanawakilishwa katika nukta tano: Kujisalimisha, kunyenyekea, kutii, Ikhlas (kuwa mkweli), na utulivu na hilo ndilo linalomhakikishia kiutendaji mwanadamu anapokuwa chini ya mwavuli wa uja ambao unakusanya ulimwengu wote, na tunaona kuwa haya maneno matano ndio maana ya Uislamu.

Maiko: Tafadhali nibainishie uliyoyasema:

Rashidi: Katika matunda muhimu ya taswira hiyo ni uhusiano wa mwanadamu na ulimwengu wake. Na kinachoakisi kwa yule aliyefuata Uislamu hisia za ndani za usalama na amani kwa nafsi yake pamoja na wanaomzunguka na kuishi kwake kwa msingi wa umoja, nalo linamrahisishia yeye kuhama kutoka kwenye hisia za umoja kuelekea kwenye umoja wa kihisia hadi kwenye umoja wa kutengeneza mfumo na kupatikana hali ya ulinganisho katika maisha yake, ulinganisho unaochunga pande zote za ubinadamu; kiroho, kiakili na kimwili.

Kama ambavyo Muislamu anaefahamu kuwa Mwenyezi Mungu ndie aliyetujulisha kuwa ametuumba na kutuumbia vyote vilivyomo ardhini:

{Yeye ndiye aliye kuumbieni vyote vilivyomo katika ardhi…} [2:29] na akasema: {Na amefanya vikutumikieni vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika ardhi, vyote vimetoka kwake. Hakika katika hayo zimo Ishara kwa watu wanao fikiri} [45:13], anajua kuwa Mwenyezi Mungu hakutuumba na kutudhalilishia kisha tusiwe na uhusiano wowote! Ni lazima mahusiano ya mtu yawe wazi pamoja na yale yaliyodhalilishwa na Mwenyezi Mungu kwa ajili yake, ikiwa hali ndivyo ilivyo hapana budi basi Mwenyezi Mungu kuteremsha elimu inayohukumu mahusiano haya kati ya mwanadamu na vitu hivi kwani Mwenyezi Mungu amesema: “Hakika Mola Mlezi wenu ni Mwenyezi Mungu aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Kisha akatawala juu ya Kiti cha Enzi….” (7:54), na akasema vilevile: “Ati binaadamu anadhani kuwa ataachwa bure? ”(75:36), Yaani anafanya katika ulimwengu huu bila ya vidhibiti vya maamrisho na makatazo, na ikiwa ni hivyo, basi hapana budi Muislamu kujifunza na kufanya utafiti kuhusu dini yake ambayo yatamhakikishia uadilifu wa kilimwengu na wa kisheria ardhini.

Uislamu unaondoka kwenye msingi huu ili ulete mfumo kamili wa maisha, hivyo basi unaratibu uhusiano wa Muislamu na Mola wake, kama vile ibada zake na hali zake za kiroho, kama unavyoratibu maisha yake katika miamala yake; kama vile kuoa kwake na kuacha kwake, kuuza na kununua … desturi zake kama vile adabu za kula, kunywa, kulala. kuvaa, kuingia nyumbani na kutoka, hata usafi wake mwenyewe…vile vile unaratibu uhusiano wake na jamii yake, nchi yake, na jamii nyinginezo ili ihusishe nyanja zote za maisha katika sheria, uchumi, siasa, utamaduni na jamii….Hivyo Uislamu unaondoka hapo ili ujenge mfumo kamili unaohusisha nyanja zote za maisha na kuziratibu.

Dini kama ambavyo inaelekeza kwa muislamu hisia zake, hivyo hivyo imemwekea kanuni na kumsimamishia mizani za uadilifu na haki. Humuamrisha kujenga ardhi na daima kutafuta, kuvumbua kingo za ulimwengu na nafsi…yote hayo yanatokea kwenye wigo wa mahusiano na Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kumnyenyekea katika uja wake, majukumu haya ya kimaisha yakizoeleka na yakiwa yameunganishwa na mfumo wa Mwenyezi Mungu; basi wakati huo yatabadilika na kuwa ibada kwa Mwenyezi Mungu.

Maiko: Ulichokitaja ni athari ya khofu yangu katika kupetuka mipaka na kukakamaa, au sema wazi: Dini kutawala maisha.

Rashidi: Hapana budi tufahamu kuwa kila kitu kina nidhamu na utaratibu wake wa kuyaendesha mambo yake, na hivyo kila kipengele kinakuwa katika sehemu yake husika na faida zake, na kwa kuunganisha vipengele hivi kwa njia ya ukamilifu ndipo manufaa na faida ya nidhamu au mfumo huu unapopatikana na malengo yake kufikiwa, na hili ndilo aliloliita Mwenyezi Mungu mizani katika kauli yake: {Na mbingu ameziinua, na ameweka mizani, Ili msidhulumu katika mizani. Na wekeni mizani kwa haki, wala msipunje katika mizani} [55:7-9].

Mizani ni uadilifu, na mizani hii ambayo ni uadilifu inakuwa katika kila kitu, na kama ambavyo ulimwengu huu umesimama katika vipimo na makadirio na juu yake kumesimama mfumo wote na sehemu zake, hivyo basi dini hii iliyoteremshwa na Muumba imesimama vile vile katika mizani na uadilifu.

Hivyo basi, mizani na kutodhulumu haki za wengine ni sifa ya jumla katika Uislamu, hili linatafsiriwa kwa uadilifu, linganifu na usawa katika mfumo wa mwanadamu ndani ya nafsi yake na katika maingiliano ya miamala yake na wengine.

Na ulinganifu wa mwanadamu na unyoofu katika taswira yake kuhusu nafsi yake na hukumu yake mara nyingi ndio inayohukumu taswira yake kuhusu wengine na hukumu juu yake, na katika maana ya ulinganifu huu na unyoofu ni kile kilichoelezwa na Allah kuhusu waja wake wema katika dua zao: {Na katika wao wapo wanao sema: Mola wetu Mlezi, tupe duniani mema, na Akhera mema, na utulinde na adhabu ya Moto!} [2:201]

Na katika maana hii, aya tukufu zifuatazo ziliteremka:

{Na utafute, kwa aliyo kupa Mwenyezi Mungu, makaazi ya Akhera. Wala usisahau fungu lako la dunia. Nawe fanya wema kama Mwenyezi Mungu alivyo kufanyia wema wewe. Wala usitafute kufanya ufisadi katika ardhi. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi mafisadi} [28:77],

{Na wale ambao wanapo tumia hawatumii kwa fujo wala hawafanyi ubakhili, bali wanakuwa katikati baina ya hayo} [25:67]

Na,

{Wala usiufanye mkono wako kama ulio fungwa shingoni mwako, wala usiukunjue wote kabisa, utabaki ukilaumiwa muflisi} [17:29).

Maiko: Inanisikitisha vile vile kuwa mwanadamu amekuwa sasa ananyonya damu ya nduguye mwanadamu, na maadili ya watu yameharibika kiasi cha fedheha na kupelekea nguvu aliyonayo mwanadamu aliyopewa na Mwenyezi Mungu atumie kumletea tabu na kumuangamiza badala ya kuitumia katika yenye kumpelekea kwenye furaha, amani na raha …Uislamu unaangaliaje tatizo hili?

Rashidi: Hii ni nyumba ya mateso ambayo mwanadamu amejitayarishia mwenyewe kwa ajili ya nafasi yake katika dunia hii, hakuna sababu isipokuwa ni kuwa mwanadamu kwa mchezo anajaribu kutawala chombo asicho kijua muundo wake, chombo hiki cha kibinadamu hajui siri zake ila ambae amekitengeneza, na anajua tabia zake, Yeye ndie mwenye kujua kinaendeshwa vipi.

Ama hivi sasa kama mwanadamu huyu akiweza kuzuia nafsi yake katika kutekeleza wazimu huu na kuamua kufuata kanuni alizowekewa na yule aliyetengeneza chombo kile, huenda akatengeneza upya kile ambacho hadi hivi sasa ameshakiharibu, vinginevyo hakuna tiba mbadala katika aliyonayo hivi sasa kama vile misiba, maangamivu, tabu, hasara n.k.

Maiko: Wewe unakusudia kuwa hakuna uokovu isipokuwa kwa kufuata mfumo wa Kiislamu, vinginevyo wanadamu wataishi katika tabu na mashaka?!

Rashidi: Kimantiki hii ni dalili katika kiwango cha mtu binafsi na katika viwango vya kijamii, duniani na akhera; hakuna kinachowezekana katika kuweka mipaka ya ukaidi na shari za mwanadamu katika dunia hii, isipokuwa hisia zake kwa aliyokuwa nayo kama vile anayoambatana nayo na majukumu, hivyo mtu akiwa na yakini katika dunia hii kufanya atakayo na hakuna atakayemuuliza anachofanya wala kuwepo nguvu juu yake inayomfuatilia ayafanyayo, hivyo basi hakutakuwa na mpaka wa ukaidi wake na ukorofi wake, kama ambavyo hili ni sahihi yanapohusiana na mtu, vivyo hivyo ni sahihi yanapohusu familia yake au umma au wakazi wote wa ardhini, huu ni uchaguzi wetu sote, ni uchaguzi wa kukiri uja wetu, kunyenyekea kwetu kwa Mola wetu na Mfalme wetu.

Mimi na wewe na wale wote ambao Allah amewamakinisha ardhini tunapambana na uchaguzi huu, na tulikuwa tumetahiniwa akili zetu na muruwa wetu na hisia zetu kwa wajibu na ahadi yetu, ni juu ya kila mmoja kuamua; Je, ni kweli yeye ametekeleza ahadi au ni haini wa ufalme wake wa kweli?

Ama mimi nimeamua ndani ya nafsi yangu kufuata njia ya utiifu na kutii ahadi, na mimi nimetoka kwenye utiifu wowote, basi, bila shaka kila mmoja atakuwa ametoka katika utiifu wa Mwenyezi Mungu. … Kwa hakika hili ndilo bara la amani.

Maiko: Treni imefika katika kituo chake cha mwisho… haya twende. Sheria ya Mwenyezi Mungu