Abdullah Harlal Ghandi,

quotes:
  • Juu ya Vichwa vya Mashahidi.
  • “Nyote mnafahamu kuwa mimi ni “Heral” mtoto wa kiongozi mkubwa wa Kipagani, “Ghandi”. Mimi natangaza mbele ya vichwa vya mashahidi na katikati ya kundi kubwa hili la Waislamu kuwa mimi nimeupenda Uislamu, nimeipenda Qur-aan na nimemuamini Allah Peke Yake na Mtume wake mtukufu Sayidina Muhammad (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) na kuwa yeye ni Mtume wa mwisho na kuwa hakuna nabii baada yake na Qur-aan ilichokileta ni haki na vitabu vyote viliyoteremshwa ni haki. Mitume na manabii wote ni haki. Na kwa Uislamu na Qur-aan nitaishi na kufa kwa ajili yake na nitautetea na kupigana kwa ajili yake na nitakuwa moja ya nguzo yake imara na nitaulingania kati ya jamaa na ndugu zangu. Dini hii tukufu ni dini ya elimu, utamaduni, uadilifu, uaminifu, rehama na usawa.”