MISINGI YA UWEKAJI SHERIA

MISINGI YA UWEKAJI SHERIA

MISINGI YA UWEKAJI SHERIA

$Arnold_Toynbee.jpg*

Arnold J. Toynbee

Mwanahistoria wa Uingereza
Ujumbe wa Utume wa Muhammad.
“Muhammad alitumia muda wake wote kufanikisha ujumbe wake katika kudhamini hizi mandhari mbili katika mazingira ya jamii yake ya kiarabu, hayo mawili ni Umoja katika Fikra ya dini, kanuni na nidhamu ya utawala na hukumu. Yote yalitimia kwa fadhila za nidhamu ya Uislamu ambayo ulibeba mgongoni mwake umoja na utawala wenye mamlaka kwa pamoja. Uislamu ukawa na nguvu kwa fadhila hiyo, nguvu yenye msukumo na utisho imewahamisha waarabu kutoka kwenye umma wa kijahili na kuwa ulioendelea.”

Uwekaji sheria wa Kiislamu umesimama katika misingi na nguzo za aina yake ambazo zinamfaa mwanadamu yeyote wa zama na mahala pote, na misingi ile muhimu ni hii ifuatayo:

Kuwepesisha

Majukumu yote ya kisheria hayatoki nje ya uwezo wa wale waliokalifishwa na nafasi yao, wala haimbebeshi mtu mzigo au kumtoa katika mazoea katika kazi za kawaida, kwani dini ni nyepesi, Allah Mtukufu amesema: “…Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito…” (2:185),

Na Allah tena akasema: “Mwenyezi Mungu anataka kukupunguzieni taabu, na mwanaadamu ameumbwa dhaifu.” (4:28),

Na tena Allah Mtukufu akasema: “Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo…” (2:286).

$George_Sarton.jpg*

George Sarton

Muhadhiri wa Vyuo Vikuu vya Washington na Harvard.
Akida iliyokita.
“Katika nguzo tano za Uislamu hakuna kitu kinachochukiwa na asiyekuwa Muislamu. Pamoja na wepesi wa faradhi hizi na uchache wa idadi yake, hakukuwa na haja ya kuingiza marekebisho yatakayoiongoza kwenye kuithibitisha imani ya Kiislamu katika nafsi ya kila Muislamu. Hakika ubobezi wa kielimu kwa imani ya Kiislamu ina dalili ya dhati kutokana na nguvu yake, kubakia na kuenea kwake.”

Mama Aisha (Radhiya LLahu ‘anha) amesema: “Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) hakukhiyarishwa kati ya mambo mawili ila alichagua jepesi zaidi, madamu si dhambi, ikiwa ni dhambi alikuwa mbali nayo sana, Wallahi hakulipa kisasi kwa ajili ya Nafsi yake jambo aliloletewa katu, hadi pale ambapo Sheria ya Allah itakapovukwa, hivyo kulipa kisasi kwa ajili ya Allah” (Al-Bukhari).

Miongoni mwa kuondoa uzito (Mashaka) katika sharia ya Kiislamu ni majukumu machache; kiasi cha kumuwezesha mwenye kukalifishwa kusimamia majukumu yake bila ya uchovu au taabu; kwani katika uchovu kuna mashaka na dhiki, na mashaka huondoshwa, Allah Mtukuka amesema: “…Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini…” (22:78),

Kama ambavyo malengo ya majukumu ya kisharia ni kumpelekea mwenye kutekeleza majukumu yake katika maisha ya furaha duniani na akhera, hivyo basi sharia haileti jukumu ila kulingana na kinachowezekana kwa maumbile na tabia ya mwanadamu, Allah Mtukuka amesema: “Enyi mlio amini! Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni. Na mkiyauliza inapo teremshwa Qur’ani mtabainishiwa. Mwenyezi Mungu amesamehe hayo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira Mpole. Waliyauliza hayo watu wa kabla yenu, kisha wakawa wenye kuyakataa.”(5:101-102).

Kuchunga maslahi

$Will_Durant.jpg*

Will Durant

Mwandishi wa Kimarekani.
Dini Kwanza.
“Misingi ya tabia ya Kiislamu, sheria na serikali yao. Vyote vimesimama juu ya misingi ya dini: Uislamu ni dini nyepesi zaidi na ya wazi kuliko dini nyingine. Na msingi wake ni kushuhudia kuwa hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Allah na Muhamad ni Mtume wa Allah.”

Mwenye kufuatilia hukumu za sheria ya Kiislamu itamdhihirikia kuwa muradi wake ni kufanikisha maslahi ya watu; kiasi cha kuwafanikishia watu kheri na wema, na hivyo basi kuondosha shari, ufisadi duniani na akhera, kwa mtu binafsi na kwa jamii yote katika zama na mahali pote, Allah Mtukuka amesema: “Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote.” (21:107),

Kwa hiyo rehema ni kwa ajili ya kufanikisha maslahi, vinginevyo kama rehema isingekuwa ndio makusudio yake, basi Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) asingesifika kuwa Nabii mwenye rehema, na majukumu yote yanarejea katika maslahi ya waja duniani na katika akhera yao; kwa sababu Allah anajitosha kwa waja wake wote, hivyo basi utii haumnufaishi wala maasi hayamdhuru.

Sharia yote ni adilifu, ina kila aina ya huruma, maslahi na hekima; na suala lolote lililotoka kwenye uadilifu kwenda kwenye dhuluma, kutoka kwenye dhuluma na rehema kwenda kinyume chake, na kutoka kwenye maslahi kwenda kwenye uharibifu na ufisadi, na kutoka kwenye hekima kwenda kwenye upuuzi hayo si katika sharia.

Uadilifu

Maandiko mengi yameshirikiana kuthibitisha nafasi ya Uadilifu kama mfumo wa jumla kwani tunapata maandiko yenye kulingania kusimamisha uadilifu, na mengine yenye kukataza dhuluma, hata ikiwa ni pamoja na mtu mwenye kuhalifu, Allah Mtukuka amesema: “Enyi mlio amini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mkitoa ushahidi kwa haki. Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamngu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.” (5:8).

Ukamilifu wake

Kwa hakika miongoni mwa yanayoonesha kusihi dini hii ni kule kujipambanua kwa upana na ukamilifu wake, Allah Mtukuka amesema: “…Hatukupuuza Kitabuni kitu chochote…” (6:38),

Na akasema vile vile: “…Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinacho bainisha kila kitu, na ni uwongofu, na rehema, na bishara kwa Waislamu.” (16:89),

Na kuenea huku kunaonekana katika akida na taswira, na katika ibada na kujikurubisha, na katika Akhlaki na fadhila, (ubora katika maeneo yote) na katika uwekaji sheria, oganaizesheni na hukumu mbali mbali, si hivyo, bali katika maisha yote.

Dini ya kati na kati

Dini ya Uislamu ni dini ya usawa na ulinganifu: “Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wa wasitani…” (2:143),

$Naseem_Sousa.jpg*

Naseem Souza

Mhadhiri wa Kiiraqi, Myahudi
Uislamu… Ni amani na salama.
“Mayahudi chini ya bendera ya Uislamu walipata amani na uadilifu ambayo iliwazuia na shari ya uadui na kukandamizwa, na Karne nyingi zilipita wakiwa katika kheri nyingi.”

Na kila kitu katika hukumu zake zimetayarishwa katika mizani makini: “Na mbingu ameziinua, na ameweka mizani” (55:7)

Na Allah amewaamrisha Waislamu kusawazisha kila kitu, miongoni mwa hayo kauli yake Allah Mtukuka: “Na wale ambao wanapo tumia hawatumii kwa fujo wala hawafanyi ubakhili, bali wanakuwa katikati baina ya hayo” (25:67),

Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) amekataza Ghuluu (kupetuka mipaka): Akasema:

“Tahadharini kuzidisha katika dini kwani (ghulu) kuzidisha imewaangamiza waliokuwa kabla yenu.”

Na akaamrisha usawa na kumpa kila mwenye haki, haki yake. Amesema Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam): “Hakika Mola wako ana haki juu yako, na Nafsi yako ina haki juu yako, na kwa familia yako ina haki juu yako, hivyo mpe kila mwenye haki haki yake.”