KUUMBWA NA KUKIRIMIWA KWA MWANADAMU

KUUMBWA NA KUKIRIMIWA KWA MWANADAMU

Kuumbwa na kukirimiwa kwa mwanadamu

Kumkirimu mwanadamu

$027_1.jpg*

%%

Tone katika Bahari
“Hadi hivi sasa nyota kubwa iliyoumbuliwa ni VY Canis Majoris iko mbali nasi kwa masafa ya miaka elfu tano ya mwanga na ni kubwa kuliko jua kwa 9,261, 000,000 yaani 9 Bilioni na mara 261 milioni!! Na jua ni kubwa kuliko ardhi yetu kwa mara 1,300,000.

Pamoja na utukufu wa umbile la mbingu na ardhi isipokuwa ni kwamba Mwenyezi Mungu amemdhalilishia hilo mwanadamu na kujaalia vitu hivyo kudhalilika kwake: Pamoja na utukufu wa umbile la mbingu na ardhi isipokuwa ni kwamba Mwenyezi Mungu amemdhalilishia hilo mwanadamu na kujaalia vitu hivyo kudhalilika kwake: “Na amefanya vikutumikieni vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika ardhi, vyote vimetoka kwake….” (45:13);

Na hilo ni kwa kumkirimu yeye mwanadamu na kumfadhilisha yeye kuliko viumbe vingine vyote, Allah Ta’ala amesema: “Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba.” (17:70)

Allah amemuumba mwanadamu na kumjulisha kisa cha kuumbwa kwa Adam na kukirimiwa, kisha kumteremsha kutoka peponi kushuka ardhini kwa wasiwasi wa shetani na dhambi zake, kisha kutubia kwake, Allah amesema: “Na hakika tulikuumbeni, kisha tukakutieni sura, kisha tukawaambia Malaika: Msujudieni Adam. Basi wakasujudu isipo kuwa Iblisi, hakuwa miongoni mwa walio sujudu. Mwenyezi Mungu akasema: Nini kilicho kuzuia kumsujudia nilipo kuamrisha? Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, naye umemuumba kwa udongo. Akasema: Basi teremka kutoka humo! Haikufalii kufanya kiburi humo. Basi toka! Hakika wewe u miongoni mwa walio duni. Akasema: Nipe muhula mpaka siku watakapo fufuliwa. Akasema: Utakuwa miongoni mwa walio pewa muhula. Akasema: Kwa kuwa umenihukumia upotofu, basi nitawavizia katika Njia yako Iliyo Nyooka. Kisha nitawazukia mbele yao na nyuma yao na kuliani kwao na kushotoni kwao. Wala hutawakuta wengi wao wenye shukrani. Akasema: Toka humo, nawe umekwisha fedheheka, umekwisha fukuzwa. Hapana shaka atakaye kufuata miongoni mwao, basi nitaijaza Jahannam kwa nyinyi nyote. Na wewe, Adam! Kaa wewe na mkeo katika Bustani hii, na kuleni humo mpendapo. Wala msiukaribie mti huu, mkawa katika wale walio dhulumu. Basi Shet’ani aliwatia wasiwasi ili kuwafichulia tupu zao walizo fichiwa, na akasema: Mola Mlezi wenu hakukukatazeni mti huu ila msije mkawa Malaika, au msije mkawa katika wanao ishi milele. Naye akawaapia: Kwa yakini mimi ni miongoni wa wanao kunasihini. Basi akawateka kwa khadaa. Walipo uonja ule mti, tupu zao zilifichuka na wakaingia kujibandika majani ya Bustanini. Mola wao Mlezi akawaita: Je, sikukukatazeni mti huo, na kukwambieni ya kwamba Shet’ani ni adui yenu wa dhaahiri? Wakasema: Mola wetu Mlezi! tumejidhulumu nafsi zetu, na kama hutusamehe na kuturehemu, hakika tutakuwa katika wenye kukhasirika. Akasema: Teremkeni! Mtakuwa nyinyi kwa nyinyi maadui. Na kwenye ardhi itakuwa ndio makao yenu na starehe yenu mpaka ufike muda. Akasema: Humo mtaishi, na humo mtakufa, na kutoka humo mtatolewa. ” (7:11-25)

Mwenyezi Mungu amempa mwanadamu sura nzuri kabisa, kisha akampulizia roho yake, hivyo mwanadamu akatokea katika umbile zuri kabisa anasikia na kuona na kutembea na kuzungumza: “…Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji.” (23:14)

Na akamfundisha kila anachohitaji kukifahamu na akampa sifa na vipawa ambavyo hakumpa kiumbe mwingine kama vile: Akili, Elimu, ubainifu, kuongea, umbile, sura nzuri, umbile lililokirimiwa na kiwiliwili cha kati na kati, na kuweza kupokea elimu mbalimbali na kutumia dalili kwa fikra na kuongoza katika tabia njema na sifa nzuri kabisa na akamkirimu na kumfadhilisha kuliko viumbe vingi; katika mandhari ya kukirimiwa hivi kwa mwanadamu iwe kwa mwanamume au mwanamke.

Mada ya kwanza katika tangazo la kimataifa la haki za binadamu.

Binadamu wote ni sawa.
“Watu wote huzaliwa huru wakiwa sawa katika utukufu na haki, na wamepewa akili na dhamira. Na ni juu yao kuamiliana baadhi yao kwa wengine kwa roho ya udugu.

-Hakika Allah amemuumba mwanadamu kwa mkono wake tokea kuumbwa kwake wakati wa kuumbwa kwa Adam (‘Alayhi Salaam); na huu ni utukufu na kukirimiwa hakuna utukufu zaidi ya huu; Allah Ta’ala amesema: “Mwenyezi Mungu akamwambia: Ewe Iblisi! Kipi kilicho kuzuia kumt’ii yule niliye muumba kwa mikono yangu? Je! Umejiona mkubwa, au umekuwa katika wakuu kweli?” (38:75)

-Hakika Allah Ta’ala amemuumba mwanadamu katika umbile zuri; Allah amesema, “Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa.” (95:4)

Na akasema vile vile: “…na akakupeni sura, na akazifanya nzuri sura zenu. Na marudio ni kwake” (64:3).

-Mwenyezi Mungu Mtukufu amemkirimu mwanadamu huyu wa kuamrisha Malaika wake kumsujudia Adam, Baba wa wanadamu, aliposema Allah Ta’ala: “Na pale tulipo waambia Malaika: Msujudieni Adam. Wakamsujudia isipo kuwa Iblisi….” (17:61).

-Allah Ta’ala amemkirimu mwanadamu huyu na akamneemesha kwa akili, kufikiria, kusikia, kuona na hisia nyingine za fahamu, Allah Ta’ala amesema: “Na Mwenyezi Mungu amekutoeni matumboni mwa mama zenu, hali ya kuwa hamjui kitu, na amekujaalieni masikio na macho na nyoyo ili mpate kushukuru.” (16:78).

-Allah Ta’ala alimpulizia roho; na hapo ndipo daraja lake likawa la juu, Allah akasema: “Na nitakapo mkamilisha na kumpulizia roho inayo tokana nami, basi muangukieni kwa kumt’ii.” (38:72)

Na huu ni ukarimu mkubwa alioupata mwanadamu; na ndipo ilipopasa mwanadamu kuheshimiwa kama mwanadamu, sasa iweje mwanadamu huyu amfanyie uadui yule aliyempulizia roho Allah Ta’ala.?!!

$sahabi.jpg*

Ribi’I bin ‘Amir

Miongoni mwa sahaba wa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam)
Ujumbe wetu
“Allah ametutuma kuwatoa watokao kwenye kuabudu watu kuelekea kwenye kumuabudu Allah. Na kutoka katika mashaka ya dunia kuelekea kwenye upana wake, na kutoka kwenye dhuluma ya dini kwenda kwenye uadilifu wa Uislamu”

Allah Ta’ala akamfanya kuwa ni Khalifa katika ardhi, na sio Malaika au Jini; Allah akasema: “Na pale Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Mimi nitamweka katika ardhi Khalifa (mfwatizi), wakasema: Utaweka humo atakaye fanya uharibifu humo na kumwaga damu, hali sisi tunakutakasa kwa sifa zako na tunakutaja kwa utakatifu wako? Akasema: Hakika Mimi nayajua msiyo yajua.” (2:30)

Na huu ni utukufu mkubwa ambao Malaika hawakuupata ambao hawamuasi Allah alichowaamuru, na ambao daima wapo katika kumdhukuru, kumtakasa na kumtukuza Allah Ta’ala.

-Allah Ta’ala amemdhalilishia mwanadamu huyu yote yaliyomo hapa ulimwenguni kwa mbingu zake na ardhi yake, na yaliyomo baina yake na ndani yake katika jua, mwezi, nyota na sayari. Allah Ta’ala amesema: “Na amefanya vikutumikieni vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika ardhi, vyote vimetoka kwake. Hakika katika hayo zimo Ishara kwa watu wanao fikiri. ” (45:13),

-Kuwa Allah Ta’ala amemkomboa mwanadamu na amemuacha huru na utumwa wowote kwa kiumbe chochote (kingine) kadiri ya ubora wake au ukubwa wake, na hicho ni kilele cha uhuru aliokuwa nao mwanadamu; kwa jinsi alivyohamishwa kutoka katika kunyenyekea kwa mwanadamu na kumuabudu mwanadamu mwenzake hadi kumuabudu Allah Ta’ala, na kuabudu huku kwa ajili ya Allah ndio kilele cha uhuru dhidi ya kumuabudu asiyekuwa Yeye. Na hii ndio maana Allah akakataa kuwepo kwa wakala baina yake na waja wake; kwani kuna baadhi ya watu wamejiwekea na kuzusha wakala baina ya mwanadamu na Mola wake na wengine kwa hilo wamepewa sifa ya Uungu. Allah amemkirimu mwanadamu kwa sababu hakuna wakala baina yake na Mola wake, Allah amesema: “Wamewafanya makuhani wao na wamonaki wao kuwa ni marabi badala ya Mwenyezi Mungu, na pia Masihi bin Maryamu. Na wala hawakuamrishwa isipo kuwa wamuabudu Mungu Mmoja, hapana mungu ila Yeye. Subhanahu, Ametakasika na hayo wanayo mshirikisha nayo.” (9:31).

-Kumkomboa mwanadamu kutokana na khofu ya mustakbali na kukata tamaa, nayo ni kwa kupitia kuamini kwa hukumu (majaliwa) na kudura pamoja na kufuata sababu zote za kimaisha za kimaada; hivyo basi imani ya majaliwa na kudura ndio inayomfanya mwanadamu muumini katika hali ya usalama na amani, na katika hali ya utukufu na hisia ya karama na kuondokana na kero na huzuni au masikitiko yaliyopita madamu hakufanya mapungufu katika kuchukua na kutumia sababu mbali mbali. Kwa sababu yote ni kutoka kwa Allah, Allah Ta’ala amesema¨ “Hautokei msiba katika ardhi wala katika nafsi zenu ila umekwisha andikwa katika Kitabu kabla hatujauumba. Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi.” (57:22),

Imani hii inamfanya mwanadamu kuwa katika mizani nzuri ya nafsi na utulivu mkubwa wa kweli; ambapo misiba haimuathiri wala haimfanyi kuwa muoga au mwenye huzuni kama ambavyo neema mbalimbali na furaha haimfanyi kuwa ni jeuri, mwenye kujiona na kujivuna

-Akili ya mwanadamu kuheshimiwa; Allah Ta’ala ameipa thamani kubwa sana akili ya mwanadamu pamoja na fikra zake Ameamuru kuangalia na kuchukua mazingatio, na kajaalia swala la kufikiria kuhusu kuumbwa kwa mbingu na ardhi na kusimamisha hoja na dalili mbali mbali kuwa ni faradhi; Allah Ta’ala amesema: “Sema: Angalieni yaliomo mbinguni na kwenye ardhi! Na Ishara zote na maonyo hayawafai kitu watu wasio amini.” (10:101)

$Etienne_Denier.jpg*

Etienne Denier

Mchoraji na Mwanafikra wa Kifaransa
Hakuna mtu wa Kati
“Kuna jambo muhimu: Nalo kutokuwepo mtu wa kati baina ya mja na Mola wake. Na hili ndilo walilolipata wenye akili za kitendaji.”

Kadhalika Allah ameamuru akili ya mwanadamu iheshimiwe, kutunzwa, kuangaliwa vizuri, kuifanyisha kazi, kuishughulisha, na kutoyagandisha kwa njia ya kufuata mambo kibubusa na kutumia kasumba tu; Hakuna kukalifishwi ila kwa kutumia akili, kama vile ambavyo Mwenyezi Mungu alivyofanya akili ya mwanadamu kuwa ndio dalili ya kuwepo kwake Yeye Allah na hoja ya upweke wake; bali Allah amewataka wanadamu warejee kwenye akili pale wanapotofautiana; Allah Ta’ala amesema: “…Sema: Leteni ushahidi wenu kama nyinyi ni wasema kweli” (2:111)

Na akaikomboa akili kutokana na kila aina ya upotofu, ushirikina, udajali na kutegemea majini na mfano wa hayo.

-Kuhakikisha na kuthibitisha kuwa kila mwanadamu ana majukumu (wajibu) na atahesabiwa kwa matendo yake, wala hakuna uhusiano wowote na matendo ya mtu mwingine, Allah Ta’ala amesema: “Na mbebaji habebi mzigo wa mwingine…” (35:18)

Na kukirimiwa huku kwa mwanadamu ndani ya Qur-aan; kunafuta ile fikra ya dhambi ya asili, na kumkomboa na kumsafisha mwanadamu kutokana na mazito yake.

Mwanamke ni kama mwanamme kwa kukirimiwa

Kukirimiwa mwanadamu hakukuishia tu kwa mwanamume bila ya mwanamke, au kwa jinsia moja bila ya nyingine, asili ya mwanamke ni sawa na ya mwanamume katika kukirimiwa na kutukuzwa sawa kwa sawa: “…Nao wanawake wanayo haki kwa Sharia kama ile haki iliyo juu yao….” (2:228)

$Oxford-Uni.jpg*

%%

Sawa kwa Sawa
“Chuo kikuu cha Oxford hakijatoa haki sawa baina ya wanafunzi wa kike na wa kiume (katika Michezo na Umoja wa wanafunzi); isipokuwa kwa uamuzi uliotolewa tarehe 21 Julai mwaka 1964.”

Allah Mtukufu akasema: “Na Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki walinzi….” (9:71),

Wala mwanamke hatofautiani kabisa na mwanamume katika suala la malipo ya akhera, Allah amesema: “Mola Mlezi wao, akayakubali maombi yao akajibu: Hakika sipotezi kazi ya mfanya kazi miongoni mwenu, akiwa mwanamume au mwanamke, kwani ni nyinyi kwa nyinyi….” (3:195),

Na katika aya nyingine, Allah kasema: “Na anaye fanya mema, akiwa mwanamume au mwanamke, naye ni Muumini - basi hao wataingia Peponi wala hawatadhulumiwa hata kadiri ya tundu ya kokwa ya tende.” (4:124)

$Roger_Garaudy.jpg*

Roger Garoudye

Mwanafalsafa wa Kifaransa
Muujiza ya kweli
“Ikiwa sisi tutalinganisha misingi ya Qur’ani na misingi ya jamii zote zilizopita; basi tutakuta kuwa Qur-aan ndio itakayokuwa imerikodi maendeleo ndani yake yasiokuwa na ubishi, na haswa haswa kwa munasaba wa Athens na Roma; ambapo mwanamke alikuwa na mapungufu kwa sura thabiti.”

Allah amemkirimu mwanamke kama mwanadamu pindi alipo mzingatia kuwa ni mwenye kukalifishwa mwenye majukumu kamili kama alivyo mwanaume na ni mwenye kulipwa thawabu na kuadhibiwa kama alivyo mwanaume, hata jukumu la mwanzo kabisa ambalo Mwenyezi Mungu amempa mwanadamu lilikuwa la wote kwa pamoja; yaani mwanamke na mwanaume; pale Allah alipowaambia wanadamu wa mwanzo ambao ni Adamu na mke wake: “Na tulisema: Ewe Adam! Kaa wewe na mkeo katika Bustani, na kuleni humo maridhawa popote mpendapo, lakini msiukaribie mti huu tu; mkawa katika wale walio dhulumu.” (2:35)

Kama ambavyo Allah hakumbebesha mzigo mwanamke kuwa ndiye aliyekuwa sababu ya kumtoa Adam peponi na tabu walizokuwa wakipata au kuendelea kuzipata vizazi vyao baada yao kama ilivyo katika dini nyinginezo, bali Allah amemtaja Adam kuwa ndie mhusika mkuu: “Na hapo zamani tuliagana na Adam, lakini alisahau, wala hatukuona kwake azma kubwa.” (20:115) “Basi wakaula wote wawili, na uchi wao ukawadhihirikia na wakaanza kujibandika majani ya Bustani. Na Adam akamuasi Mola wake Mlezi, na akapotea njia. Kisha Mola wake Mlezi akamteuwa, naye akamkubalia toba yake, naye akamwongoa. ” (20:121-122).

%%

Mwanamke katika Sheria za mwanadamu
“Huko Roma kulikuwa na mkutano mkubwa, ukitafiti mambo ya mwanamke. Maamuzi yakatolewa kuwa mwanamke hana roho (nafsi) na kwa sababu ya dosari hii hatarithi maisha ya akhera. Kadhalika mwanamke ni uchafu hapaswi kula nyama, wala kucheka, bali hata kuzungumza, na muda wake wote autumie katika swala, ibada na utumishi. Wakamkataza kufanya yote hayo wakamwekea kufuli la chuma mdomoni mwake; ikawa mwanamke katika familia za juu na za chini anatembea njiani na akienda na kurudi nyumbani kwake na huku mdomoni mwake kukiwa na kufuli. Hii ni mbali na mateso mengine ya kiwiliwili ayapatayo mwanamke huyu kwa kumzingatia kuwa yeye ni nyenzo ya upotoshaji anayotumia shetani kuharibu nyoyo.”

Hivyo basi katika utu na ubinadamu ni kuwa mwanaume analingana na mwanamke sawa kwa sawa, Allah Ta’ala amesema: “Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari. ” (49:13)

Hivyo ni kuwa mwanaume anashirikiana na mwanamke na wanafanana au wako sawa kwa sawa katika mambo yafuatayo:-

%%

Mwanamke mbele yao
Katika sheria za kale za Kihindi tunasoma: Maradhi, mauti, moto, sumu, nyoka na moto vyote hivyo ni bora kuliko mwanamke. Haki ya mwanamke ya kuishi huisha kwa kuisha haki ya mumewe ambae ndie bwana na mmiliki wake. Akiona maiti yake inaungua nae hujitupa kwenye moto ule, vinginevyo ni haki yake kupata laana ya milele.

-Maendeleo ya mtu katika haki maalum za kumiliki: Haiba ya mwanamke ni yenye hadhi na kuheshimiwa kisheria, Allah amempa haki sawa na mwanaume katika Majukumu na utekelezaji wake, amemthibitishia haki yake ya kutumia na kuingia katika mkataba yote; kama haki ya kuuza, haki ya kununua na mfano wake, na haki zote hizi ni za wajibu kutekeleza bila ya kifungo chochote au kizuizi ambacho kitazuia uhuru wake wa kutekeleza, ila vizuizi vile ambavyo vina mzuia mwanaume vile vile, Allah Tabaaraka amesema: “…Wanaume wana fungu katika walio vichuma, na wanawake wana fungu katika walio vichuma…” (4:32),

Kadhalika amempa haki ya kurithi, Allah Ta’ala amesema: “Wanaume wana sehemu katika wanayo yaacha wazazi na jamaa walio karibia. Na wanawake wanayo sehemu katika waliyo yaacha wazazi na jamaa walio karibia. Ikiwa kidogo au kingi. Hizi ni sehemu zilizo faridhiwa.” (4:7)

$Aristotle.jpg*

Aristotle

Mwanafalsa wa Kigiriki
Ni Jeuri gani hii?!!!
“Mwanamke kwa mwanamume ni kama mtumwa kwa bwana wake. Au ni kama vile kazi za mikono ukilinganisha na kazi za akili. Au ni kama mfano wa Mshenzi na Myunani. Mwanamke ni mwanamume mpungufu, ameachwa amesimama katika daraja la chini kwenye ngazi ya maendeleo.”

Na akamfanya mwanamke mbele ya sheria sawa na mwanaume anapopatia au kukosea; Allah amesema: “Na mwizi mwanamume na mwizi mwanamke, ikateni mikono yao, hayo ni malipo ya waliyo yachuma, ndiyo adhabu ya mfano itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima.” (5:38).

-Malipo ya Akhera; Allah amesema: “Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini, tutamhuisha maisha mema; na tutawapa ujira wao kwa bora ya waliyo kuwa wakiyatenda.” (16:97)

%%

Mwanamke wa Kifaransa
“Huko Ufaransa moja katika majimbo yake kulifanyika mkutano mwaka 586 mazungumzo yalihusu mwanamke: Je, ni mwanadamu au sio mwanadamu? Hitimisho lilikuwa ni uamuzi wa waliohudhuria kuwa mwanamke ni binadamu, lakini ameumbwa kumuhudumia mwanamume, katika mwezi wa Februari mwaka 1938 ilitolewa kanuni ya kufuta kanuni zingine zilizokuwa zikimkataza mwanamke wa Kifaransa katika baadhi ya matumizi ya mali (baada ya hapo kuruhusu) na kwa mara ya kwanza katika historia ya mwanamke wa Kifaransa aweze kufungua akaunti kwa jina lake katika mabenki.

Urafiki na kunusuriana. Allah amesema: “Na Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki walinzi. Huamrisha mema na hukataza maovu, na hushika Sala, na hutoa Zaka, na humt’ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hao Mwenyezi Mungu atawarehemu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mtukufu Mwenye nguvu, Mwenye hikima.” (9:72).

-Yamekuja maamrisho ya kumhurumia mwanamke na kumfanyia wema; Allah ameharamisha wanawake kuuwawa katika vita, na akaamrisha kukaa pamoja na wanawake wenye hedhi na kufanyia nao uwakala na wakati huo Mayahudi walikuwa wanakataa hilo na kuwatenga na kuwadharau wala hawafanyi nao uwakala hadi watoharike, mwanamke katika zama za Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) walikirimiwa kwa hali ya juu pindi aliposema: “Mbora wenu ni mbora wenu katika familia yake, na mimi ni mbora wenu kwa familia yangu.” (Imepokewa na Tirmidhi, na akasema hadithi hii ni Hassan Sahihi).

$1155177_44220441.jpg*

Kitabu Kitakatifu- Agano la kale

Haki za Mwanamke Zimemezwa
“Nikageuka, na moyo wangu ulikazwa katika kujua na kupeleleza, na kuitafuta hekima, na maana ya mambo yaliyoko; ili nifahamu ya kuwa uovu ni upumbavu, na upumbavu ni wazimu. Nami nimeona lililo na uchungu kupita mauti; yaani, mwanamke ambaye moyo wake ni mitego na tanzi, na mikono yake ni kama vifungo.” (Mhubiri 7:26)

-Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) alikasirika pale mwanamke alipopigwa katika zama zake, na kusema: “Mmoja wenu anampiga mke wake kipigo cha mtumwa, kisha jioni humkumbatia” (Al-Bukhari).

-Na wakati kundi la wanawake lilipokuja kuwashitaki waume zao kwa Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam); Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) alisema: “Wanawake wengi wamekuja katika nyumba ya Muhammad kuwashitakia waume zao, wao (waume) hawakuwa bora kwao.” (Abu Dawuud).

$Mona_Mc_Cluskey.jpg*

Mona Cluskey

Mwanadiplomasia wa Kijerumani
Sawa kwa Sawa
“Katika kivuli cha Uislamu mwanamke amerejesha uhuru wake, na akapata hadhi ya juu: Uislamu unawazingatia wanawake kuwa ni ndugu walio sawa na wanaume, na kila mmoja anamkamilisha mwingine, Uislamu umelingania taaluma ya mwanamke na kumzawadia elimu na utamaduni. Kwa hiyo ukampa haki ya kumiliki na uhuru wa kutumia anachomiliki, kama ambavyo umempa haki ya kuvunja mkataba wa ndoa na uhuru wa kufikiri na kujieleza.”

Mwanamke amepewa ambayo hajapewa mwanaume; Allah ameamrisha mama afanyiwe wema zaidi kuliko baba wakati mmoja mtu mmoja alikuja kwa Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) akasema: “Ewe Mtume wa Allah ni nani mwenye haki ya kusuhubiana nae –katika riwaya nyingine wema –Mtume akasema: Mama yako, akauliza: Kisha nani? Akasema: Mama yako, akauliza: Kisha nani? Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) akasema: Baba yako.” (Al-Bukhari na Muslim).

$King_Henry_VIII.jpg*

Mfalme Henry wa Nane

Sheria za Mwanadamu zinadhulumu na ni jeuri
“Mfalme Henry wa nane alitoa kanuni ya kuharamisha mwanamke kusoma kitabu kitakatifu. Kama ambavyo mwanamke alikuwa akihesabiwa katika Sheria za jumla za Kiingereza katika mwaka 1850 kuwa si katika raia wake wala hawakuwa na haki zao binafsi, wala hata haki ya kumiliki nguo zao wala katika mali zao walizopata kwa jasho lao.”

Na hivyo Mtume kuyafanya malezi ya watoto wa kike yana ujira mkubwa kuliko malezi ya watoto wa kiume; Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam) amesema: “Atakayejaribiwa (kuwa) na wasichana hawa kisha akawafanyia wema, watakuwa sitara yake na moto” (Bukhari na Muslim)

Na akaseme tena Mtume (Swala Llahu ‘alayhi wasallam):

“Ewe Mola kwa hakika mimi nasikitishwa (kwa kutotolewa) haki za wanyonge wawili; yatima na mwanamke” (Hadithi Hassan, imepokewa na An-Nasai kwa sanad nzuri)